Hati hiyo imetafsiriwa kwa Kiswahili na Zaina Foundation.
Hati asili: Risks: Things you should know before running OONI Probe
Kwa uelewa wetu, hakuna mtumiaji wa OONI Probe ambaye amepata madhara kutokana na kutumia programu yetu. Kwahiyo, Hatari zilizoelezewa ni za kinadharia na za kusadikika. Unapotumia OONI Probe katika “mazingira yenye hatari kubwa” tunakushauri kusoma taarifa zetu hapa chini.
Mtu yeyote anayefuatilia shughuli zako mtandaoni (kwa mfano. Mtoa huduma za mtandao, serikali, mwajiri) wataweza kukuona wakati unapotumia OONI Probe;
Web Connectivity test cha OONI huunganisha na kupakua data kutoka kwa tovuti mbalimbali, ikiwemo tovuti za uchochezi na zisizokubalika (kwa mfano. Tovuti za ngono), ambazo zinaweza kuwa ni kinyume na sheria za baadhi ya nchi;
Pale tu, vipimo vyote vya mitandao vinapokusanywa na OONI Probe huchapishwa ili kuongeza uwazi wa udhibiti wa mtandao, ili kukuza mijadala ya umma, na kuwezesha tafiti. Hata hivyo, kutuma taarifa za mtandao wa ndani kwa seva za kigeni kunaweza kusitazamwe vyema na baadhi ya serikali. Wakati data zilizochapishwa ili kutambua udhibiti wa mtandao (na tunajitahidi tuwezavyo kutochapisha anwani za IP), Watoa huduma za mtandao waliohamasishwa wanaweza kujaribu kutambua watumiaji wa OONI Probe kupitia data ya umma ya OONI.
Hivyo basi hatari zinazoweza tokea wakati wa kutumia OONI Probe hutegemeana na:
Hali yako ya vitisho. Mwanaharakati mashuhuri anakuwa katika uangalizi mkubwa, kwa mfano, anaweza kushawishi kufuatiliwa zaidi anapotumia OONI Probe.
Sheria na miongozo ya nchi unayotumia OONI Probe. Ni vyema kuwashirikisha wanasheria wa ndani, na kujifunza kama nchi hiyo ina historia ya kuwashtaki watu binafsi wanaojihusisha na aina kama hizo za shughuli.
Aina ya vipimo vya OONI Probe unavyofanya. Sio kila kipimo cha OONI Probe kina hatari sawa inayoweza kutokea. Kwa mfano kipimo cha WhatsApp cha OONI, mara chache huweza kuunganisha ambazo tayari zimeunganishwa na watu zaidi ya bilioni duniani kote. Unaweza kuchagua kipimo vipi ufanye kupitia programu ya OONI Probe.
Aina ya tovuti unazopima. Unaweza kuchagua tovuti unazozipenda kupitia kitufe cha “Choose websites” katika programu ya OONI Probe ya simu, au kwa kutumia OONI Run. Pia unaweza kuchangia orodha ya vipimo kwa kupendekeza URLs zinazopaswa kuongezwa au kuondolewa.
Ikiwa una data ya OONI Probe zilizochapishwa. Unaweza kuchagua kutochapisha matokeo ya vipimo vya OONI Probe kupitia programu ya OONI Probe.
Vipimo vya program ya OONI (huitwa OONI Probe) vimeundwa kupima mitandao kwa ajili ya udhibititi wa mitandao na usafirishwaji wa data kwa namna isiyo ya kawaida. Katika baadhi ya nchi, kutumia OONI Probe kunaweza kukusababishia mashtaka ya jinai, kutozwa faini, hata kufungwa. Hivyo basi tunahimiza kushauriana na mwanasheria mwenye leseni katika nchi yako kabla ya kuipakua, kuweka na kutumia OONI Probe, na kusoma kwa uangalifu nyaraka zilizopo hapa chini.
Watumiaji wa OONI Probe wanafanya vipimo kwa hatari zao wenyewe. Kwa kuweka OONI probe ili uitumie, watumiaji hukubaliana kufuata utaratibu wa leseni na Sera ya Data ya programu ya OONI Probe. Siyo mradi wa OONI wala Mradi wa Tor, zinaweza kuwajibika, kwa pamoja au tofauti, kwa sheria au kwa haki, kwa watuamiaji wa OONI Probe na wengine wasiohusika moja kwa moja chini ya makubaliano, mkataba wowote au jambo lolote litakalo tokea.
Zingatia: Hatari zilizoelezewa hapa chini ni za kinadharia sana. Kwa uelewa wetu, hakuna mtumiaji wa OONI Probe ambaye amewahi kukumbana na madhara kutokana na hatari zilizoelezewa hapa chini. Hata hivyo, tunakuhimiza usome maelezo yafuatayo kuhusiana na hatari zinazoweza kutokea zinazohusiana na matumizi ya OONI Probe.
Kwa baadhi ya nchi, aina yeyote ya upimaji wa mtandao inaweza kuwa kinyume na sheria, au huchukuliwa kama ujajusi.
Serikali nyingi zina historia kubwa ya kupelekea wanaharakati wa haki za kidigitali kwenye aina mbalimbali za unyanyasaji ambao hufanya matumizi ya OONI Probe kuwa hatari katika nchi hizo. Hivyo utumiaji wa OONI Probe unaweza kupelekea watumiaji kuwa na makosa ya jinai au adhabu za fidia za kimahakama. Vikwazo hivyo vinahusisha:
Kufungwa
Mashambulio ya kimwili
Fidia kubwa
Vitisho
Kuwekwa kwenye orodha inayoangaliwa na serikali
Kulengwa kwa ajili ya kufuatiliwa
Kwa kuvitazama vitisho hivi, tunakuhamasisha kumuhusisha mwansheria na kuelewa hatari za kisheria kabla ya kutumia OONI Probe. Hatari zinazoweza kutokea ukitumia OONI Probe ni hizi hapa chini.
Watumiaji fulani wanaweza kupata adhabu kama watumiaji hao watagundulika na wahusika wa tatu (kama vile serikali) ambao hutazama OONI Probe kama tishio.
Utumiaji wa OONI Probe unaweza kugundulika na watu wasiohusika moja kwa moja kupitia.
Watu wasiohusika moja kwa moja (kama vile serikali, mtoa huduma wako wa mtandao, au muajiri wako) anaweza akafuatilia baadhi au vitu vyote unavyovifanya kwenye mtandao. Hii inaweza kuwaruhusu kugundua usafirishaji wa taarifa kupitia mtandao utokanao na utumiaji wako wa OONI Probe na kuihusiaha hii na wewe binafsi.
Nchi nyingi hutumia programu za kisasa za ufuatiliaji ambazo huruhusu serikali kufatilia shuguli za watu za mtandaoni-Licha ya kutumia huduma za faragha kama vile Tor, Psiphon, VPN, au seva za proxy. Katika nchi hizo, serikali au watu walio husika moja kwa moja wanaweza kukutambua wewe kama mtumiaji wa OONI Probe bila kujali mbinu gani umezitumia kulinda faragha yako ya mtandaoni.
Huduma zilizounganishwa na OONI Probe zinaweza kuona anwani zako za IP na zinaweza kugundua kuwa unatumia OONI Probe. Unaweza kuona huduma zipi hupimwa na OONI Probe hapa.
Kama ilivyo katika programu nyingine yeyote, utumiaji wa OONI Probe unaweza kuacha alama. Kwa yeyote anayefikia compyuta yako kwa karibu au mbali anaweza kuona kuwa umepakua, umeweka na kutumia OONI Probe.
Moja kwa moja,vipimo vyote vilivyotokana na OONI Probe hutumwa kwenye kikusanya cha vipimo na kuchapishwa kupitia:
Matokeo yake, umma-wakiwemo watu walio husika moja kwa moja ambao hutazama utumiaji wa OONI Probe kama tishio-wataweza kuona vipimo vyote vya mtumiaji, isipokuwa kama watumiaji hawata chagua kupitia mpangilio wa programu ya OONI Probe.
Data zilizochapishwa zitahusisha kadirio la eneo lako, mtandao (ASN) uliojiunganisha nao, na muda uliotumia OONI Probe kufanya vipimo. Vilevile hutambua taarifa, kama vile anwani yako ya IP, haijakusanywa kwa makusudi, lakini inaweza kujumuishwa katika Header za HTTP au metadata zingine. Kurasa iliyojaa maudhui iliyopakuliwa na OONI Probe inaweza ikawa na taarifa hizo , kwa mfano, tovuti ina misimbo ya ufuatiliaji au maudhui yaliyomo katika eneo la mtandao wako. Utambuzi wa taarifa unaweza kuwawezesha watu wasiohusika moja kwa moja kukutambua kama mtumiaji wa OONI Probe.
OONI imetengeneza programu nyingi za vipimo, ambapo kila moja imetengenezwa kufanya kazi tofauti. Hivyo basi, vipimo hivi huwa na hatari kwa mtumiaji.
Kwa ujumla, OONI Probe imetengenezwa kwa ajili ya:
Kupima kama tovuti zimezuiliwa;
Kupima kama program ujumbe wa hapo hapo (IM) programu za WhatsApp au ujumbe za Facebook zimezuiliwa;
Kutambua uwepo wa mifumo (kifaa kinachoingilia kati mawasiliano) ambayo inaweza kusababisha udhibiti, ufuatiliaji, na usafirishaji wa data usio wa kawaida;
Kuchunguza vifaa vya kukwepa udhibiti kama kama vile Tor na Psiphon zimezuiliwa.
Tunatamani upitie viainisho na maelezo kwa kila kipimo cha OONI Probe kwa umakini kabla ya kuvitumia.
Unapofanya kipimo cha upatikanaji tovuti cha OONI unajiunganisha na kupakua data kutoka katika tovuti mbalimbali zilizopo katika orodha mbili zifuatazo:
Orodha maalum ya vipimo ya nchi (tafuta katika orodha ya vipimo vya nchi yako kwa kuzingatia msimbo wa nchi)
Orodha ya vipimo ya dunia (hujumuisha orodha ya tovuti zinazopatikana duniani)
Tovuti nyingi zilizoorodheshwa hapo juu zina utata na zinaweza kujumuisha ngono au kauli za chuki. Maudhui haya yanaweza kuwa kinyume na sheria kuyapata katika nchi yako. Baadhi ya nchi, upatikanaji wa maudhui ambayo ni kinyume na sheria yana madhara makubwa, kama vile kifungo. Hivyo basi tunapendekeza kuwa makini kwa kutambua kama upo tayari kuchukua tahadhari ya kupakua data kutoka kwenye tovuti hizo kupitia vipimo vya OONI Probe.
Ikiwa huna uhakika na matokeo ya kujiunganisha na kupakua data kutoka kwenye tovuti zilizo orodheshwa hapo juu, unaweza kuchagua tovuti zipi za kupima kupitia kitufe cha “Choose Website” katika Programu ya OONI probe ya simu au kwa kutumia OONI Run.
Baadhi ya vipimo vya mtandao vilivyofanywa na OONI Probe zinaweza kukiuka sheria ya matumizi ya kompyuta katika nchi yako au masharti ya mtoa huduma wako wa mtandao.
Hususani, waendeshaji wa mtandao walioathiriwa na vipimo vya OONI Probe wanaweza kuona vipimo hivi kama mashambulizi. Kipimo cha OONI cha HTTP-invalid-request-line, kwa mfano, kinaweza kusababisha mashaka unapotuma jumbe zisizo maalum katika huduma ya kurudisha data iliyopokelewa kutoka katika chanzo chake na inaweza kutazamwa kama aina ya “udukuzi”. Kama vipengele vya mtandao vimeathiriwa na kipimo hiki hutazama jumbe hizi ambazo sio maalum kama mashambulizi, unaweza kupata madhara makubwa kama vile mashtaka chini ya sheria ya matumizi mabaya ya kompyuta.
Vipimo vyetu vya uchunguzi wa mtandao (NDT) ni kipimo kinachofanywa kwa lengo kuu ya kuchunguza seva za watoa huduma wengine wasiohusika moja kwa moja kupitia Maabala ya vipimo (M-Lab). Huduma za NDT za M-Lab’s zinahitaji udhibiti na usiri wa anwani za IP kwa lengo la utafiti. Kwa taarifa zaidi kuhusiana na usimamizi wa data wa M-Lab utazipata kupitia maelezo ya faragha.
Hatari za kisheria kupakua, kuweka na kutumia OONI Probe zinaweza kutofautiana kati ya nchi na nchi, ndio maana tunakushauri uombe muongozo wa mwanasheria mwenye leseni katika nchi yako.
Baadhi ya maswali unayoweza kumuuliza mwanasheria wako yahusianayo na matumizi ya OONI Probe ni:
Je nchi yangu imenizuia kutumia:
Programu za kupima mtandao?
Programu za kutambua Udhibiti?
Programu za kukwepa udhibiti?
Je ni kinyume cha sheria kutumia tovuti fulani?
Je kuna sheria katika nchi yangu ambazo zinahitaji watoa huduma wa mtandao kufuatilia shughuli zangu mtandaoni?
Je kuna mtu yoyote nchini kwangu amewahi kutuhumiwa kutokana na shughuli zao za mtandaoni? (sio lazima kuwa mahususi kwa vipimo vya mtandao)
Zingatia, orodha hii ya maswali haikuzuii kuuliza maswali mengine.
Kwa kuongeza, wakati nchi nyingi hazina sheria mahususi zinazozuia matumizi ya programu za kupima mtandao, matumizi ya OONI Probe yanaweza kuwa ni kosa la jinai kwa baadhi ya chini ya sheria zingine pana. Kwa mfano, kutumia OONI Probe kunaweza kuonekana kama kinyume cha sheria au shughuli iliyo kinyume na serikali. Watumiaji wa OONI Probe pia wanaweza kuwa na hatari ya kutuhumiwa kwa misingi ya usalama wa taifa kama data zilizopatikana na kuchapishwa kupitia OONI Probe zitaonekana kama “zinahatarisha” usalama wa nchi ndani na nje. Pia unaweza kuhitaji kuomba ushauri kwa wanasheria kuhusiana na hili.
Zaidi, kuomba ushauri kwa mwanasheria, pia unaweza kuwasiliana nasi ukiwa na maswali husika kwa contact@openobservatory.org. Tafadhali, kumbuka kwamba, sisi sio wanasheria, na taarifa yoyote tunayokupa haihusishi ushauri wa kisheria. Kwa kuongezea, mawasiliano yako nasi hayalindwi na hayana kinga kisheria kwahiyo mamlaka inaweza kutoa wito na kuhitaji taarifa zote ulizotupatia. Hata hivyo tunaweza kukuunganisha na wanasheria wenye uwezo wa kujibu maswali yako.
Baadhi ya vyanzo muhimu ni:
Zingatia: Vyanzo hivi havina ushauri wa kisheria na inaweza kuwa imepitwa na wakati. Tafadhali hakikisha unasoma toleo la hivi karibuni kabla ya kuchukua ushauri wowote.
Pia, watumiaji wa OONI Probe hufanya hivyo kwa hatari zao wenyewe. Kwa kuweka OONI probe ili uitumie, watumiaji hukubaliana kufuata utaratibu wa leseni na Sera ya Data ya programu ya OONI Probe. Siyo Mradi wa OONI wala Mradi wa Tor, zinaweza kuwajibika, kwa pamoja au tofauti, kwa sheria au kwa haki, kwa watumiaji wa OONI Probe na wengine wasiohusika moja kwa moja chini ya makubaliano, mkataba wowote au jambo lolote litakalo tokea.