Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (MYM)

Hati hiyo imetafsiriwa kwa Kiswahili na Zaina Foundation.

Hati asili: Frequently Asked Questions (FAQ)

Kipengele hiki kimelenga kuonyesha Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (MYM) na jamii.

Kuna maswali mengine ambayo ungependa tuyajibu? Tafadhali tujulishe.

Kuhusu OONI

OONI ni nini?

Open Observatory of Network Interference (OONI) ni mradi wa programu huru ambao umelenga kuwezesha juhudi katika kuongeza uwazi wa udhibiti wa mtandao ulimwenguni.

Tangu mwaka 2012, OONI imetoa Programu kadhaa za vipimo vya udhibiti (OONI Probe) na imechapisha vipimo vya mtandao zaidi ya bilioni katika mtandao.

Kwa nini OONI?

Unaweza kutumia programu , njia za wazi na data za wazi kuthibitisha matokeo yetu, kuzalisha tafiti zingine kutokana na tafiti etu na kuchunguza udhibiti wa mtandao katika nchi yako.

Tumetengeza OONI ili kuwezesha mijadala ya umma pamoja na kutoa taarifa zenye ushahidi na kufanya uchechemuzi katika taarifa zinazodhibitiwa.

OONI inafanya nini?

Kuwezesha juhudi katika kuongeza uwazi wa udhibiti wa mtandao ulimwenguni, tuna:

Kwa nini kupima udhibiti wa mtandao?

Udhibiti wa mtandao unaweza kupelekea uvunjifu wa haki za binadamu (kama vile haki ya uhuru wa kujieleza na kupata taarifa).

Japokuwa, kutambua udhibiti wa tovuti na huduma uliokusudiwa unaweza kuwa mgumu. Hizi ni miongoni mwa sababu:

  1. Ni vigumu kutambua udhibiti wa tovuti na huduma ambazo hazijulikani zaidi. Udhibiti wa mtandao ni rahisi kutambua pale zinapoathiri huduma ambazo tumezoea kutumia, au tovuti hizo zinaporipotiwa na vyombo vya habari. Udhibiti wa Telegram na Instagram uliotokea Iran, kwa mfano,uliripotiwa na vyombo vya habari na kupewa usikivu kimataifa, wakati Udhibiti wa tovuti za kidini na za kikabila zinaweza zisijulikane.

  2. Udhibiti wa mtandao kwa kawaida hutofautiana katika mitandao ndani ya nchi. Kwenye nchi nyingi, watoa huduma za mitandao huzuia upatikanaji wa mtandao katika tovuti, na mara nyingi hutokana na maagizo ya serikali yasiokuwa na maelezo. Tovuti inaweza kupatikana kwenye mtandao mmoja na isipatikane kwenye mitandao mingine.

  3. Njia nyingi za udhibiti ni ngumu kuzitambua. Watoa huduma za mtandao wanapokuletea kurasa iliyozuiliwa, kwa kawaida wanakujulisha kuwa kurasa hiyo imekusudiwa kudhibitiwa na mara nyingi huambatanisha na maelezo ya kisheria. Baadhi ya watoa huduma wengine wanaweka kurasa tupu ambapo inakua na utata kuweza kutambua kama imekusudiwa kudhibitiwa au haipatikani kwa sababu zingine (kama vile tatizo la kiufundi). Katika nchi nyingi, watoa huduma za mtandao hawaweki kurasa tupu kabisa. Isipokuwa, wanadhibiti tovuti kwa njia mbalimbali (Kudhibiti jina la kikoa, au kudhibiti anwani ya IP au kuingiza RST), ambapo hawataarifu watumiaji wala kufafanua kuhusu udhibiti huo. Kwa kesi hizi ni vigumu kutambua kama imekusudiwa kudhibitiwa au haipatikani kwa sababu zingine (mtandao kutokua hewani au tatizo la DNS iliyokosewa kusajiliwa).

  4. Baadhi ya watoa huduma za mtandao hutumia mbinu mbalimbali za udhibiti. Wakati mtoa huduma wako anaweza kudhibiti kurasa za baadhi ya tovuti (na kukutaarifu kuwa tovuti hizo zimekusudiwa kudhibitiwa) wanaweza kuzuia tovuti tofauti kwa mbinu tofauti pamoja ili kuzuia uwezo wako wa kutambua udhibiti wa tovuti nyingine. Baadhi ya nchi, vilevile watoa huduma wanazuia tovuti moja kwa mbinu tofauti.

  5. Udhibiti na uharibifu uliopitiliza. Kwa mfano Indonesia, Vimeo na Reddit zilipatikana zimedhibitiwa japokuwa zilishaondolewa zaidi ya miaka miwili iliyopita. Misri, tovuti kadhaa ambazo ziliendeshwa katika CDN hiyo hiyo Kama ilivyokuwa Arab Mpya pia ilidhibitiwa.

  6. Kiuhalisia tovuti au huduma isiyopatikana haimaanishi kuwa imedhibitiwa na mtoa huduma wako. Inaweza kuwa imeendeshwa na seva isiyo ya uhakika, au mmiliki wa tovuti/huduma amedhibiti anwani za IP zote kutoka kwenye nchi ambayo unajaribu kuipata (kwa kuzingatia sheria na miongozo)

Hivyo basi, upimaji wa udhibiti wa mtandao, ni muhimu kwa sababu inaturuhusu kukagua mtandao na kugundua sababu za kwa nini na kivipi hatuwezi kujiunganisha na huduma ya mtandao.

Wanapokagua mtandao tunaona, kwa mfano mtoa huduma wako anadukua anwani ya IP ya tovuti ambayo unajaribu kuipata, taarifa hii inaweza kuwa muhimu kutoa ushahidi wa udhibiti uliokusudiwa kutokana na uwezo wetu wa kupata tovuti ilyokusudiwa.

Kwa kutumia OONI Probe, unaweza kupima mitandao na kukusanya data zinaonyesha nini kimedhibitiwa, kwa namna gani, lini na nani.

Ni kwa namna gani OONI inafadhiliwa?

Kama ilivyo miradi mingi ya taasisi zisizo ingiza faida duniani, kimsingi OONI inaendeshwa kupitia ruzuku na michango.

Baadhi ya wafadhili wetu wakuu ni Bureau of Democracy, Human Rights, and Labor (DRL) na Ford Foundation.

Kwa miaka mingi Open Technology Fund (OTF) amekua mfadhili wetu mkuu, mwanzoni aliwezesha kazi za kwanza za OONI mwaka 2012. OTF waliwezesha baadhi ya miradi ya programu maarufu ambazo zinaimarisha haki za binadamu kwenye mtandao kama vile Tor na Signal.

Tumepokea msaada kutoka Mozilla (Mozilla Open Source Support) ili kuboresha OONI Explorer. Awali uanzishwaji wa OONI explorer (mwanzoni ilizinduliwa mwezi wa tatu mwaka 2016) iliwezeshwa na Wizara ya mambo ya nje ya German. Kwa miaka mingi tumekuwa tukipokea msaada kutoka kwa baadhi ya taasisi nyingine pia, kama vile Media Democracy Fund (MDF), Internet Society (ISOC), na National Science Foundation (NSF).

Vilevile tumepokea aina nyingine za msaada, kama vile michango kutoka kwenye kampuni kama Google Jigsaw, Pantheon, Netlify, AirVPN na VPNCompare. Tumepokea msaada wa miundombinu kutoka Greenhost na Amazon (kwa ajili ya kuendesha vipimo vya OONI kwenye Amazon S3 na kutumia kifaa kikubwa cha data ili kuchambua vipimo.).

Kama ungependa kuwezesha kazi zetu, tafadhali changia OONI.

Kuna uhusiano gani kati ya OONI na Tor?

OONI ilianzishwa kutokana na mradi wa Tor.

Mwaka 2011, waanzilishi wa mradi wa Tor walianza kutengeneza mbinu huru na mipango kazi kwa lengo la kupima aina mbalimbali za udhibiti wa mtandao, ndipo ikatengenezwa OONI.

Kati ya mwaka 2011 hadi 2019, OONI ni miongoni mwa miradi iliyoendeshwa chini ya mradi wa Tor. Mwaka 2020, OONI ilifadhiliwa na Kituo cha Uwazi na Haki za Kidigitali za binadamu cha Hermes, lakini tulijiendesha wenyewe kwa namna ya Harambee na utawala.

Tumeendelea kuwa sehemu ya jamii ya Tor na kushirikiana katika kupima upatikanaji wa Tor.

OONI inapatikana wapi?

OONI ni mradi wa kimataifa, unaohusisha jumuiya ya kimataifa wenye kikosi cha kimataifa.

Kwa miaka mingi wafanyakazi wa OONI wamekuwa wakitokea kwenye nchi nyingi, ikiwemo Italia, Ugiriki, Africa Kusini, Cameroon, India, Urusi, Ujerumani, na Slovenia.

Hatujajikita katika nchi yeyote, na hatujawahi kuwa ofisi na kwa kawaida tunafanya kazi kupitia mtandao.

OONI inatambulika kisheria?

OONI ni mradi usioingiza faida, lakini haujasajiliwa kisheria.

Kati ya mwaka 2011 hadi 2019, OONI ulikuwa mradi wa Tor (a501(c)(3) usio ingiza faida uliosajiliwa U.S). Mwaka 2020 tulifadhiliwa na Kituo cha Uwazi na Haki za Kidigitali za binadamu cha Hermes ambayo ni taasisi ya haki za kidigitali.

Ni kwa namna gani naweza kujihusisha na OONI?

Kuna namna nyingi ambazo unaweza kujihusisha na OONI!

OONI Probe

OONI Probe ni nini?

OONI Probe ni programu huru na ya bure iliyotengenezwa kupima udhibiti wa mtandao na aina nyingine za udhibiti wa mtandao.

Nchi yangu haina Udhibiti. Kwa nini nitumie OONI Probe?

Tunadhani ni muhimu kupima udhibiti wa mtandao katika kila nchi duniani (Bila kujali kama kuna ripoti za udhibiti wa mtandao au la) kwa sababu:

Vipimo vya OONI Probe hufanya nini?

OONI Probe inahusisha programu nyingi za upimaji zilizotengenezwa kupima:

Kwa namna gani OONI Probe inapima udhibiti wa mtandao?

Kupima udhibiti wa tovuti, OONI Probe otomatiki hufanya uchunguzi za tovuti kutoka kwenye mitandao miwili:

Matokeo yatokanayo na mitandao miwili hujilinganisha otomiki. Kama yanafanana na tovuti iliyopimwa inajulikana kama inapatikana. Hata hivyo, kama matokeo yatatofautiana, kuna uwezekano upatikanaji wa tovuti iliyopiwa imedhibitiwa.

Unaweza kujifunza namna ya kila kipimo cha OONI Probe kinavyofanya kazi kupitia anwani za hapo chini:

Pia unaweza kuangalia viainisho vya vipimo hapa: https://github.com/ooni/spec/tree/master/nettests

Mimi sina ujuzi. Ninaweza kutumia OONI Probe?

Ni kweli kabisa! Unaweza kuwa na OONI Probe kwenye simu yako (ya Android and iOS), ambayo ndio njia rahisi ya kuweza kutumia OONI Probe. Unaweza ukapima kwa kubofya kitufe!

Pia unaweza kupima kwa kutumia OONI Probe katika kompyuta , zenye muundo, UX, na sifa zinazolingana na OONI Probe katika simu.

Ninawezaje kutumia OONI Probe?

Unaweza kutumia OONI Probe katika programu zifuatazo:

Ninatumia OONI Probe: Je nitakiwa nikutumie matokeo?

Hapana haina haja. OONI Probe imeundwa kututumia majibu hapo hapo baada ya kufanya vipimo (isipokuwa kama umechagua kutoka katika mpangilio). Majibu yako huchakatwa na kuchapishwa muda huo huo.

Ni kwa mara ngapi natakiwa kufanya OONI Probe?

Mara nyingi iwezekenavyo. Udhibiti wa mtandao unaweza kutokea ghafla, wakati kudhibiti au kutodhibiti huduma za mtandao unaweza ukabadilika kulingana na wakati.

Kimsingi unaweza ukawezesha vipimo vya otomatiki katika OONI Probe.

Nitawezaje kutumia OONI Probe otomatiki?

Unaweza kuwezesha “Vipimo vya otomotiki” katika mpangilio wa OONI Probe apps.

Kwenye mipangilio hii, una uchaguzi wa kutumia OONI Probe otomatiki ukiwa umejiunganisha kwenye WiFI au kifaa chako kikiwa kinachaji.

Linux OONI Probe CLI huendelea kufanya kazi otomatiki ikiwa umeweka programu kwa kutumia .deb package.

Kwa muda gani natakiwa kutumia OONI Probe?

Kwa muda mrefu iwezekanavyo: Udhibiti wa mtandao unaweza kutokea ghafla, wakati kuzuiliwa na kutozuiliwa kwa huduma za mtandao huweza kubadilika kutokana na wakati.

Kila unapoitumia OONI Probe, unachangia vipimo kwenye kumbumbuku za umma juu ya udhibiti wa mtandao (kwa kuwa vipimo vyako huwa zinachapishwa).

Ili Kufuatilia udhibiti wa mtandao kwa usahihi zaidi katika muda fulani, inatakiwa kuitumia OONI probe kwa muda mrefu iwezekanavyo (miaka).

Nimegundua tovuti zilizodhibitiwa. ninawezaje kukwepa udhibiti huo?

Unaweza ukajaribu kukwepa udhibiti wa tovuti au programu tumizi kwa kutumia Tor Browser au VPN (kama vile Psiphon).

OONI Probe imegundua uwepo wa kifaa kinachoingilia mawasiliano katika mtandao wangu. Je hii humaanisha ninafuatiliwa?

Hapana, sio lazima.

Watoa huduma wengi wa mtandao (ISPs) hutumia vifaa vinavyoingilia mawasiliano kwa malengo mbalimbali ya kimtandao (kama vile kutunza data), wengi wao hawana lengo la ufuatiliaji au udhibiti wa mtandao.

Je Ninaweza kupima udhibiti wa mtandao nikiwa mbali katika nchi husika?

Vipimo vya OONI Probe zimetengenezwa kwa lengo la kupima udhibiti wa mtandao kwa mtumiaji wa mtandao ndani ya nchi husika. OONI Probe imetengenezwa kupima mtandao uliounganishwa na, katika nchi ambayo mtandao unapatikana.

Ukiwa unafanya vipimo mbali(Bila kuwepo katika nchi husika) - Kwa mfano, kwa kutumia VPS - utapata majibu yasiyo sahihi kwa sababu OONI Probe haijatengenezwa kufanya kazi kwa mfumo huo.

Kwa vipimo vya mbali, tunapendekeza vifaa vingine, kama vile Satellite, ambazo huchanganua mtandao katika seva inayopokea maombi na kufanya vipimo ili kutambua DNS iliyozuiliwa.

Ni aina gani wa Data OONI Probe hukusanya?

OONI Probe imetengenezwa kwa kuzingatia faragha na usalama wa mtumiaji wake. Lakini sio kifaa cha faragha. Kwa hivyo tunajaribu kuweka ukomo wa ukusanyaji wa data kwa aina za data ambazo ni muhimu kwa ajili ya kupima aina mbalimbali vya udhibiti wa mtandao.

Kwa namna ilivyoundwa, OONI Probe hukusanya:

OONI Probe haikusanyi anwani yako ya IP.

Tunaweza kukusanya anwani yako ya IP na taarifa zingine zinazo kutambulisha bila kukusudia ikiwa hii imejumuishwa katika maelezo ya HTTP au vipimo vya maelezo ya data zingine. Data hizi zinaweza kukusanywa ikiwa mtandao wa OONI Probe unapima teknolojia ya ufuatiliaji au zina maudhui maalumu. Tuna chukua hatua kwa kuondoa anwani za IP na utambulisho wa mtu binafsi kutoka katika kanzidata yetu ambayo imekusanya vipimo ili kukupunguzia hatari.

Jifunze zaidi juu utendaji kazi wa data yetu kupitia sera ya data ya OONI: https://ooni.org/about/data-policy/

Ninawezaje kuchagua kutotuma vipimo vya OONI?

Kupitia mpangilio wa programu wa OONI Probe, unaweza kwa kutowezesha mpangalio wa “Chapisha matokeo ya kiotomiki” na kutosambaza (na chipasha) vipimo vyovyote.

Kutumia OONI Probe kuna hatari gani?

Kutumia OONI Probe kunaweza kuwa hatari, kutegemea na hali ya vitisho na nchi uliyopo unapofanya kipimo cha OONI Probe.

Baadhi ya mambo ya kuzingatia:

Kujifunza zaidi juu ya hatari zinazoweza kutokea ukitumia OONI Probe tafadhali pitia nyaraka hii: https://ooni.org/about/risks/

Ninawezaje kupunguza hatari zinazohusiana na kutumia OONI Probe?

Tunalenga kukupatia machaguo mengi zaidi iwezekanavyo, ili uweze kuondoa hatari zinazoweza kutokea na kubainisha matumizi yako ya OONI Probe kulingana na namna bora kwako.

Unaweza:

Je ninaweza kutumia OONI Probe nikiwa nimewasha VPN?

Tunashauri kutotumia OONI Probe pamoja na VPN kwa sababu hautaweza kupima utendaji kazi wa mtandao wako, badala yake, utapima Mtandao wa mtoa huduma ya VPN, ambaye anaweza kuwa hajadhibitiwa.

Kutambua udhibiti wa mtandao (Kama ilivyotokea kwa watumiaji wa ndani wa mtandao), Zima VPN yako (au program yeyote inayokwepw udhibiti mtandao) na kuwezesha vipimo vya OONI Probe kufanya kazi.

Je, OONI inaweza kutoa ushauri wa kisheria?

Hapana. Sisi ni kikosi cha watengenezaji wa programu, kwahiyo hatuwezi kutoa ushauri wowote kisheria.

Tunachokifanya, Ni kusambaza baadhi ya maswali unayoweza kuwauliza wanasheria wako kuhusiana na matumizi ya OONI Probe: https://ooni.org/about/risks/#seeking-legal-advice

Kupima Tovuti

Tovuti zipi nitapima kama zimedhibitiwa kwa kutumia OONI Probe?

Unapobofya kitufe cha “Run” katika programu tumizi ya OONI Probe, Utapima tovuti yako ikijumuisha vitu hivi:

Haijalishi unatumia OONI Probe katika nchi gani, wakati wote utapima tovuti kutoka kwenye orodha ya vipimo vya tovuti vya kimataifa.

Moja kwa moja OONI Probe itatambua orodha ipi mahususi ya nchi ,kuchagua kwa ajili ya kupima kwa kuzingatia nchi ambayo kipimo cha OONI Probe kinafanyika. Kwa mfano, Ukiwa unafanya kipimo cha OONI Probe nchini Brazil, utafanya vipimo kwa tovuti zilizomo kutoka orodha ya vipimo vya tovuti kidunia na kutoka orodha ya vipimo vya tovuti vya Brazili. Ukisafiri kwenda Ujerumani na kufanya kipimo OONI Probe, Itapima tovuti kutota duniani na orodha ya vipimo za Ujerumani.

Orodha za vipimo ni nini?

Orodha za vipimo ni orodha ya tovuti zote zilizofanyiwa udhibiti wa mtandao.

Kwanini OONI Probe inatumia orodha za vipimo?

Kupima tovuti zote zilizopo mtandaoni sio rahisi, ikizingatia kwa watumiaji wa OONI Probe wanaokumbana na vikwazo katika kasi ya mtandao. Kwa hiyo tunahitaji kuweka ukomo wa katika upimaji kwa kuchagua tovuti zilizoidhinishwa.

Orodha ya vipimo inatoa faida zifuatazo:

Kwanini Programu OONI Probe haipimi tovuti zote zilizopo katika orodha ya vipimo vya tovuti?

Kutokana na vikwazo vya kasi ya mtandao, Upimaji wa moja kwa moja wa tovuti kwa kutumia OONI Probe mobile app ni ndani ya sekunde 90. OONI Probe huchagua sampuli isiyo na mpangilio wa tovuti (Kutoka orodha ya vipimo vya dunia na orodha ya vipimo katika nchi husika) na kuziunganisha kwa wingi ndani ya sekunde 90.

Program za OONI Probe ya kompyuta hupima tovuti zote (Kutoka kwenye orodha ya vipimo vya dunia na orodha ya vipimo katika nchi husika) kwa mpigo na unaweza kudhibiti idadi ya tovuti katika mpangilio wa program.

Nawezaje kubadili muda wa vipimo katika programu ya simu ya OONI Probe ili kupima tovuti nyingi zaidi?

Unaweza kupata hatua kwa hatua (ikiwa na picha screen) jinsi ya kupima tovuti (Kutoka katika orodha ya vipimo vya Citizen Lab) kupitia muongozo wa mtumiaji ufuatao:

Ninawezaje kupata orodha ya vipimo vya nchi yangu?

Orodha ya vipimo kwa kila nchi inahifadhiwa kama CSV faili katika Citizen Lab’s test list repository on GitHub.

Mafaili haya yamehifadhiwa katika mfumo ufuatao: msimbo wa nchi nukta csv. Kwa mfano, Orodha ya vipimo vya Brazil huhifadhiwa kama br.csv (Kwa kuwa “BR” ndio msimbo wa nchi ya Brazili).

Unaweza kupata orodha ya vipimo kwa nchi yako kwa kutafuta faili la CSV lenye msimbo wa nchi.

Kwanini nchi yangu haina orodha ya vipimo?

Kama huwezi kupata orodha ya vipimo vya nchi yako, Hii inawezekana orodha haipo, Hivyo basi, katika hili OONI Probe itapima tovuti zilizojumuishwa kwenye orodha ya vipimo vya kidunia.

Tafadhali tusaidie kutengeneza orodha ya vipimo katika nchi yako.

Nani huamua tovuti za zimejumuishwa katika orodha?

Mtu yeyote anaweza, orodha ya vipimo huhifadhiwa kwa uwazi katika Github na Citizen Lab kwa uwazi ili kuhamasisha jamii kupitia na kutoa mchango.

Tunakuhamasisha kupitia tovuti zipi zimejumuisha katika orodha ya vipimo na kupendekeza kuongeza URLs.

Ninawezaje kuchangia katika orodha ya vipimo?

Unaweza kuchangia tovuti kwa ajili ya kupima udhibiti wa mtandao kupitia anwani zifuatazo:

Mimi sio mtumiaji wa GitHub, Lakini ningependa kuwasilisha URLs kwa ajili ya vipimo. Ninawezaje kufanya hivyo?

Baadhi ya michango ya orodha kubwa za vipimo hutoka kwa watu ambao hawatumii GitHub (kama vile wanasayansi jamii), kwa kuwa kuweka orodha mpya ya vipimo kunahitaji uelewa wa hali ya nchi wa kijamii na kisiasa.

Kama wewe sio mtumiaji wa GitHub na ungependa kuchangia kwenye orodha ya vipimo, unaweza kufanya hivyo kupitia Test Lists Editor.

Tafadhali rejea kwenye muongozo wa kuhariri orodha ya vipomo na screencast.

Kuna tofauti gani kati ya orodha ya vipimo na orodha ya tovuti zilizozuiliwa?

Orodha ya vipimo ni orodha ya tovuti ambazo tunapima kuangalia kama zimezuiliwa.

Orodha iliyozuiliwa kwa upande mwingine, orodha ya mitandao zilizopigwa marufuku kisheria, ambazo mara nyingi huzuiliwa.

Baadhi ya serikali mara moja moja huchapisha orodha rasmi ya mitandao iliyozuiliwa (au zilizo vujisha) zenye orodha za tovuti ambazo zimepigwa marufuku kisheria katika nchi. Watoa huduma za mitandao hupokea maagizo ya kuzuia tovuti zote katika orodha hiyo, kawaida huhusisha mamia (au maelfu) ya URLs ambazo zina maudhui yaliyo kinyume na sheria za nchi hiyo (Kama vile kamari, kusambaza mafaili, maudhui ya watu wazima,n.k.).

Orodha za Vipimo, kwa upande mwingine haimaanishi kuwa ni tovuti zilizozuiliwa tu. Badala yake, hufanya kazi ya kufuatilia pale sera zinapobadilika - Ni nini hasa kinaweza kuzuiliwa au kutozuiliwa.

Wakati orodha za vipimo huweza kujumuisha tovuti ambazo zinajulikana zimezuiliwa (na hii husaidia kujua mbinu za udhibiti zilizopitishwa na ISPs), tovuti nyingi hazijazuiliwa ndani ya nchi zinapoongezwa kwenye orodha za vipimo vya mtandao.

Kwa kutumia orodha ya vipimo vya mtandao tunalenga kutambua uzuiliwaji wa tovuti (kwa kutambua uzuiaji wa tovuti ambazo zilifikiwa hapo awali), sio tu kuthibitisha hilo.

Ni aina gani za tovuti zitapimwa na OONI Probe?

OONI Probe hupima tovuti (zilizojumuisha kwenye Orodha za vipimo vya Citizen lab) ziko chini ya makundi 30 tofauti.

Makundi haya hutofautiana na taarifa za vyombo vya habari, utamaduni, na mambo yahusuyo haki za binadamu na makundi ya tovuti yenye maudhui yasiyofa, kama vile ngono (zimejumuishwa kwa sababu zina uwezekano mkubwa wa kuzuiliwa, kuwezesha mbinu za udhibiti zilizotumiwa na ISPs.)

Ninawezaje kuchagua aina za tovuti za kupima?

OONI Probe, moja kwa moja itapima tovuti zilizopo katika makundi 30 tofauti.

Unaweza kuweka kikomo cha kupima aina za tovuti husika (kwa mfano, kupima tovuti za vyombo vya habari) kwa kufuata maelekezo ya hatua kwa hatua yaliyosambazwa katika miongozo yetu kwa:

Ninawezaje kuchagua tovuti za kupima?

Unaweza kupima tovuti ya chaguo lako (kuliko tovuti zilizojumuishwa kwenye Orodha ya vipimo) kwa kufuata maelekezo ya hatua kwa hatua yaliyosambazwa katika miongozo yetu kwa:

Ninawezaje kupima orodha maalum ya URLs?

Ikiwa utapenda kupima orodha ndefu ya tovuti, kwa kuziongeza moja baada ya nyingine kwa kubonyeza kitufe “Chagua tovuti” katika OONI Probe ya simu linaweza lisiwe chaguo sahihi.

Unaweza kupima orodha maalum ya URLs hatua kwa hatua kupitia miongozo yetu katika OONI Probe ya simu.

Data za OONI

Data za OONI ni nini?

OONI data ni vipimo vya mtandao vinavyokusanywa kwa kutumia OONI Probe test.

Kwanini OONI huchapisha data?

Katika muda halisi, Tunachapisha Vipimo vya OONI Probe kutoka ulimwenguni kote ili:

OONI huchapisha data wapi?

Kwa muda huo huo, tunachapisha taarifa za vipimo ulimwenguni kote kwa kutumia:

Nawezaje kutafsiri data za OONI?

Kila usomaji wa kipimo cha OONI hutokana na kipimo cha OONI Probe. Kutegemeana na namna kipimo cha OONI Probe kinafanya kazi, kila upimaji wa OONI una mfumo maalum wa data. Kwahiyo hii hutofautiana kati ya kipimo na kipimo.

Kwa ujumla, kipimo cha OONI huwakilisha moja kati ya matokeo matatu yafuatayo:

Nawezaje kupata na kuchambua data za OONI?

Unaweza kufanya njia zifuatazo:

Tunapendekeza kuchukua data za OONI kutoka S3 bucket kama una mpango wa kufanyia kazi data nyingi za OONI (inahusisha, kwa mfano, kupakua data zote za nchi ili kupata taarifa).

Kwa kupewa vifaa vingine (kama vile OONI Explorer) kutegemea OONI API, ni bora kudhibiti matumizi ya API ili kupunguza maombi katika ya kufanyiwa kazi katika seva (kuepuka kuathiri utendaji kazi wa vitu vingine unaotegemea seva hiyo).

OONI Explorer

OONI Explorer ni nini?

OONI Explorer ni chanzo cha wazi cha data za udhibiti wa mtandao duniani kote. Kina zaidi ya matokeo ya vipimo vya OONI bilioni yaliyokusanywa toka nchi zaidi ya 200 tangu mwaka 2012. Kila siku, mamia elfu ya vipimo vipya vya OONI huchapishwa kwa uwazi katika OONI Explorer duniani kote.

Kwa namna gani naweza kuzipata kurasa zilizo zuiliwa kwa kutumia OONI Explorer?

Unaweza kuona tovuti ziliyozuiliwa hivi punde duniani kote kwa kufuata hatua zifuatazo:

  1. Tembelea OONI Explorer

  2. Bofya “Search” (kona ya kulia juu)

  3. Chagua “Confirmed” ( chini ya “Status” katika sehemu ya kuchuja upande wa kushoto)

  4. Bofya “Filter Results

Vipimo vyote vya OONI Explorer vitachujwa na kuonyesha zile tovuti zilizothibitishwa kuzuiliwa pekee duniani kote ( kulingana na vipimo vya OONI Probe).

Kuangalia tovuti ambazo zinaweza kuwa zimezuiliwa:

  1. Bofya “Search” (juu kona ya mkono wa kulia wa OONI Explorer)

  2. Chagua “Anomalies” ( chini ya “status” katika sehemu ya k)uchuja kushoto

  3. Bofya “Filter Results

Hata hivyo, tafsiri matokeo haya kwa tahadhari sababu yanaweza yasiwe sahihi.

Nawezaje Kupata Vipimo?

Unaweza kupata vipimo vya OONI ( yaani majibu ya kipimo cha OONI Probe) kupitia hatua zifuatazo:

  1. Tembelea OONI Explorer

  2. Bofya “Search” (juu kona ya kulia)

Katika kila mstari sasa utaona (katika kurasa ya kutafuta) – msimbo wa nchi yako, tarehe za ASNs na jina la kipimo- kwa kila kipimo kimoja (matokeo ya kipimo cha OONI Probe).

Kwa mfano:

OONI measurement

  1. Bofya kila kipimo ili kukifungua.

Mfano wa kurasa ya kipimo:

OONI measurement page

Nawezaje kupata data za OONI kupitia OONI Explorer?

Ukishusha chini kurasa ya kipimo cha OONI (mfano kurasa ya kipimo), utaona data za vipimo ambazo bado hazijachakatwa - ambazo pia unaweza ukazipakua katika mfumo wa JSON.

Data za kipimo cha mtandao vitatofautiana kulingana na Kipimo cha OONI Probe kwa ambavyo ilitengenezwa.

Nawezaje kupata “ushahidi wa udhibiti wa mtandao” katika vipimo?

Kwanza kuna mambo mawili ya kuzingatia:

Kwa kuzingatia hili, unaweza kupata ushahidi wa kuzibitiwa kwa mtandao kwa urahisi kwa kufuata hatua zifuatazo:

  1. Bofya “Search” (upande wa kulia juu kwenye kona ya OONI Explorer)

  2. Chagua “Confirmed” (chini ya “Status” katika sehemu ya kuchuja kushoto)

  3. Bofya “Filter Results

Vipimo vyote vya OONI vitachujwa ili kukuonyesha watoa huduma wa mtandao duniani wenye kurasa zilizozuiliwa katika tovuti. Matokeo yataorodheshwa katika matukio ya hivi karibuni, na moja kwa moja yatawekwa katika vipimo vipya kila siku.

  1. Bofya katika kipimo

Mfano wa kipimo “imethibitishwa kuzuiliwa”:

Confirmed blocked measurement

  1. Shusha chini ili kuona data za vipimo vya mtandao ambazo hazijachakatwa.

Raw measurement data

Unaweza kupakua data katika mfumo wa JSON.

Kama ilivyo katika hatua za hapo juu, unaweza pia kupata matukio ya udhibiti wa mtandao kwa kuchagua “Anomalies” (badala ya “Confirmed”) chini ya kipengele cha “Status” katika eneo la kutafuta la OONI Explorer. hata hivyo , kuthibitisha matukio hayo yote ni ngumu na inaweza kuwa vizuri kama utamshirikisha mhandisi.

Nawezaje kupata tovuti zilizozuiliwa katika nchi?

Unaweza kuzipata tovuti zilizo zuiliwa katika nchi yako kwa kufanya yafuatayo:

  1. Tembelea OONI Explorer

  2. Bofya “Search” (juu kona ya kulia)

  3. Chagua nchi yako kupitia orodha ya nchi itakojitokeza upande wa kushoto

  4. Chagua “Web Connectivity” kupitia “Test Name”

  5. Chagua “Anomalies” na/au (chini ya status")

  6. Bofya “Filter Results

Tafadhali tafsiri matokeo “yasiyo ya kawaida” ambayo yanaweza kuwa sio sahihi.

“Iliyothibitishwa” matokeo ya uzuiaji yatatokea kama watoa huduma za mtandao waliopimwa watakuwa na kurasa zilizozuiliwa katika tovuti husika.

Nawezaje kuangalia kama tovuti husika imezuiliwa?

Unaweza kuangalia kama tovuti husika (kama vile twitter.com) huzuiliwa kwa kufuata hatua zifuatazo.

  1. Tembelea OONI Explorer

  2. Bofya “Search” (kona ya kulia juu)

  3. Chagua “Nchi” kupitia orodha ya nchi inayojitokeza upande wa kushoto

  4. Chagua “Web Connectivity” kupitia orodha ya “Test Name” itakayojitokesha

  5. Aina ya kikoa (mfano, twitter.com) cha tovuti katika mpangilio wa “Domain”

  6. Chagua “Anomalies” na/au “Confirmed” (chini ya “Status”)

  7. Bofya “Filter Results

Tafadhali tafsiri matokeo “yasiyo ya kawaida” kwa tahadhali sababu yanmaweza yasiwe sahihi.

Matokeo ya “iliyothibitishwa” kuzuiliwa yatatokea tu kama watoa huduma za mitandao waliopimwa zina kurasa zilizozuiiliwa katika tovuti husika.

Kwanini siwezi kupata majibu ya Tovuti husika?

Kama unatafuta matokeo yahusuyo tovuti fulani, (kwa kuzingatia maelekezo ya jibu lililopita) na hupati majibu yoyote, inaweza kuwa ni kwa sababu zifuatazo:

Nawezaje kuangalia uzuiliwaji wa tovuti katika muda husika?

Ili kupata matokeo ya muda husika, tumia OONI Explorer katika njia zifuatazo:

  1. Bofya “Search” (kona ya juu kulia)

  2. Chagua nchi kwa kutumia orodha ya nchi itakayotokeza

  3. Chagua “Web Connectivity” kupitia orodha ya “Test Name” itakayotokeza

  4. Bainisha kipindi cha muda kwa kuchagua tarehe za “From” na “Until” katika kalenda

  5. Chagua “Anomalies” na/au “Confirmed (chini ya hali)

  6. Bofya “Filter Results

Tafadhali tafsiri matokeo “yasiyo ya kawaida” kwa tahadhali sababu yanaweza yasiwe na usahihi.

“Iliyothibitishwa’ matokeo ya kuzuiliwa yatatokea pale ambapo watoa huduma wa mtandao waliojaribiwa wataleta kurasa zilizozuiliwa katika tovuti husika.

“Iliyothibitishwa” inamaanisha nini?

Vipimo “huthibitisha kuzuiliwa” pale ambapo tunakuwa na uhakika kabisa chanzo kilichopimwa kimezuiliwa. Kulingana na utafiti wetu wa sasa, hii hutumika kwa tovuti ambazo watoa huduma wa mitandao huleta kurasa zilizo zuiliwa (ambayo humtaarifu mtumiaji kuwa tovuti imezuiliwa kwa kukusudiwa) au ambapo seva ya DNS hurudisha majibu yenye IP iliyozuiliwa.

Kwa kuchagua “Iliyothibitishwa” kupitia OONI Explorer, utaona matokeo yote ya vipimo vya OONI yanathibitisha uzuiliwasji wa tovuti duniani kote.

Nazijua tovuti zingine nyingi zilizo zuiliwa kwanini hazionekani katika Explorer ya OONI ninapochagua “iliyothibitishwa”?

Chaguo la “Iliyothibitishwa” italeta matokeo ya (tovuti zilizozuiliwa) kama tu, haya yote yafuatayo, yatakuwepo:

Kwakuwa wakati wote tunaboresha tafiti zetu katika kugundua udhibiti, haya mambo yanabadilika kwendana na wakati. Kwa taarifa zaidi za kiufundi tembelea ooni/pipeline.

Kwanini OONI huthibitisha udhibiti wakati inapoletwa kurasa iliyo dhibitiwa?

Kurasa iliyozuiliwa ni kurasa ya tovuti ambayo humtaarifu mtumiaji kuwa tovuti aliyokusudia imezuiliwa kwa makusudi. Mara nyingi, kurasa iliyozuiliwa hutoa taarifa za uhalali wa kufungiwa kwake hata za kisheria. Kwahiyo hakuna ugumu katika aina hii ya udhibiti, kwa sababu hata watoa huduma wa mitandao huwa wazi kuhusiana na kusudi la kuzuiliwa kwa tovuti husika.

Mfano wa kurasa ya tovuti iliyowekwa na watoa huduma wa mitandao Indonesia:

Indonesian block page

Vilevile, kurasa zilizo zuiliwa huwa na alama za utambulisho wa kipekee na huwekwa katika kazidata zetu. Pale tunapoitambua alama za utambulisho wa kipekee kurasa iliyozuiliwa zimewekwa katika kazidata yetu, tunaweza kukagua kwa haraka kwa kuzitafuta katika vipimo vingine vyote ambavyo vina alama hizo za kipekee. Na matokeo yake, tunaweza kugundua uzuiliwaji wa tovuti nyingine.

Kwanini OONI huthibitisha matukio mengine ya udhibiti wa mtandao (zaidi ya kurasa zilizo zuiliwa)?

Matukio ya aina nyingine za udhibiti (kama vile kucheza na DNS au TCP/IP) ni ya kutatiza sana, kwa sababu watoa huduma ya mtandao hawamtaarifu kwa uwazi mtumiaji kuwa upatikanaji wa tovuti husika umezuiliwa (kama wanavyofanya katika kurasa zilizo zuiliwa).

Vilevile, kuna sababu nyingi zaidi kwanini matukio haya huonekana kama ni udhibiti lakini kiuhalisia siyo (ambayo husababisha utambuzi wa moja kwa moja kuwa mgumu). Kwa mfano, kipimo kilichofanyika katika mtandao usio imara unaweza kuleta dosari katika TCP/IP, ambayo haihusiani na uzuiliwaji wa makusudi wa TCP/IP. Pia inaweza kuwa tovuti iliyopimwa inaendeshwa na seva isiyokuwepo, au mmiliki wa tovuti anazuia upatikanaji wa anwani ya IP ambayo inatokana na nchi husika. Au DNS isiyo ya kawaida imejitokeza kama matokeo ya DNS isiyosanidiwa, tofauti na uzuiliwaji wa DNS wa makusudi.

Kwahiyo ni muhimu mara zote kuchunguza kila kipimo kwa kila tukio ili kukagua data kwa umakini na kujua sababu halisi kwanini kipimo chake hakijafanikiwa.

Moja kwa moja katika kutofautisha matukio ya udhibiti wa makusudi na yale ya sababu za mtandao kutokuwa wa kawaida imekuwa ni changamoto inayoendelea, japokuwa tunaendelea kufanya maboresho katika tafiti na ugunduzi wetu na kupanga kuwa na uthibitishwaji wa moja kwa moja wa aina tofauti za udhibiti wa mtandao hivi karibuni.

“Isiyo ya kawaida” inamaanisha nini?

Kipimo “kisicho cha kawaida” ni matokeo ya upimaji ambayo ni maalum sababu huwasilisha viashiria vya udhibiti wa mtandao (kama vile kuzuiliwa kwa tovuti au programu au uwepo wa kifaa kinachoingilia mawasiliano).

Inapogundulika uwepo wa kurasa iliyozuiliwa, OONI hutambulisha hivo vipimo kama “imethibitishwa” . matukio mengine yote ya udhibiti wa mtandao (kama vile kucheza na DNS au TCP/IP) hujumushwa katika vipimo “visivyo vya kawaida”.

Hata hivyo, kipimo kisicho cha kawaida sio lazima kuwa na ushahidi wa udhibiti wa mtandao, kama inavyokuwa katika majibu yasiyo na usahihi.

Kimsingi, kipimo kisicho cha kawaida, huashiria uwepo wa kitu kisicho sawa na tunatakiwa kuchunguza kwa kina data za vipimo kujua nini kinaendelea.

Kwanini OONI Explorer inasema kuwa tovuti au programu ninayotaka kutembelea imezuiliwa katika nchi yangu?

Kuna sababu mbili kwa nini hii inatokea:

  1. Labda tovuti au program husika ilizuiliwa na watoa huduma wengine katika nchi yako na siyo na mtoa huduma wako wa mtandao.

  2. Majibu ya kipimo sio sahihi. Maswali mawili yafuatayo na majibu na yameelezea hii zaidi.

Majibu yenye makosa ni yapi?

Majibu yenye makosa ni matokeo ya kipimo cha OONI Probe (kitambulika kama “isiyo ya kawaida”) ambayo kwa makosa huonyesha uwepo wa kudhibitiwa kwa mtandao (kama vile kuzuiliwa kwa tovuti au programu).

Katika kupima upatikanaji wa tovuti, OONI Probe hulinganisha matokeo kutoka katika mtandao wako na matokeo kutoka mtandao mwingine usio na udhibiti. Kama matokeo hayalingani, basi matokeo husika ya OONI Probe yatatambulika kama “siyo ya kawaida” kuonyesha uwepo wa udhibiti wa mtandao, matokeo haya yasiyo ya kawaida kiuhalisia huwa udhibiti wa mtandao, japo baadhi huweza kuwa sio sahihi.

Kwanini majibu yenye makosa hutokea?

Majibu yenye makosa hutokea kutokana na sababu kadhaa.

Zifuatazo ni sababu ambazo huchochea majibu yasiyo sahihi kutokea katika upimaji wa tovuti:

Katika kutumia kipimo cha ujumbe wa papo kwa papo cha OONI Probe (WhatsApp, Facebook Messenger, Telegram), majibu yenye makosa huweza kutokea kama mtoa huduma wa programu ya ujumbe wa papo kwa papo akifanya mabadiliko katika miundombinu yake ambayo inaathili upimaji unaoendelea.

Katika kutumia kipimo cha Kifaa kinachoingilia kati mawasiliano cha OONI Probe. Majibu yenye makosa huweza kutokea kutokana na matatizo katika uendeshaji wa miundombinu ya seva ya OONI Probe.

Katika kukutumia kipimo cha OONI Probe, majibu yasiyo sahihi huweza kutokana na matatizo ya ghafla yanayosababishwa na uundwaji wa kifaa chako au miundombinu ya mtandao wako.

Nawezaje kutofautisha majibu yenye makosa?

Kutofautisha majibu yenye makosa mara nyingi huwa ni vigumu. Inahitaji kuchunguza data za vipimo kwa uangalifu, kuwa na uelewa mzuri wa namna kipimo cha OONI Probe kinafanya kazi, kuchambua data za muda mrefu (kuangalia kama chanzo kilichopimwa huwa na tabia ya kuleta majibu yasiyo ya kawaida katika mtandao huo huo), na kutathimini na kuona sababu nyingine zinazoweza kusababisha hali hiyo (kwa mfano kuangalia kiwango cha tovuti hiyo kushindwa kidunia).

Kama sehemu ya Program ya ushirika na OONI, tunatoa msaada wa kuchambua data katika taasisi zinazotetea haki za kibinadamu ambazo tunashirikiana nazo. Data na OONI na njia za utendaji kazi zote zipo wazi na zinapatikana tukitarajia uchambuzi mwingine za data utasaidia jamii pia.

Tunakuhamasisha kuwasiliana nasi kupitia (barua pepe au slac) kama huna uhakika na kipimo na kupanga kutumia (kwa mfano) kama sehemu ya kutoa taarifa.

Kwa ujumla, tunapendekeza kupitia matokeo kwa kila muda, kuliko ya wakati mmoja tu (isipokuwa kama) yametambulika kama “yamethibitishwa”). Kwa mfano kama umegundua kwamba tovuti iliyopimwa inawasilisha hali isiyo ya kawaida ileile (kwa mfano kuchezewa kwa DNS) kila ikipimwa katika mtandao husika katika nchi, kuna uwezekano kuwa upatikanaji wake umedhibitiwa, hata hivyo kipimo kimoja, (kwa mfano) huwakilisha hali isiyo ya kawaida kwa TCP, lakini vipimo vingine vyote katika tovuti hiyo vilifanikiwa, kuna uwezekano kuwa majibu ya kipimo ya TCP isiyo ya kawaida yana makosa.

Nawezaje kuangalia matokeo kutoka vipimo vingine vya OONI Probe?

Unaweza kuchuja OONI Explorer kupata majibu kutoka katika vipimo vingine vya OONI Probe kupitia hatua zifuatazo:

  1. Bofya “Search” (kuna ya kulia juu)

  2. Siyo ya lazima: Chagua nchi kupitia orodha ya “nchi” itakayojitokeza

  3. Chagua kipimo cha OONI Probe kupitia orodha ya “Test Name” itakayojitokeza kushoto

  4. Siyo ya lazima: Chagua “Anomalies”

  5. Bofya “Filter Results

Tafadhali tafsiri matokeo “yasiyo ya kawaida” kwa tahadhali kwa sababu yanaweza kuwa na makosa.

Kwanini nchi yangu haina vipimo vyovyote vya hivi karibuni katika OONI Explorer?

Moja kwa moja OONI Explorer huchapisha matokeo ya vipimo ya watumiaji wa OONI Probe kwa wakati huo huo, ndani ya dakika baada ya kufanya majaribio.

Kama hakuna vipimo vya hivi punde kutoka nchini kwako, hii humaanisha:

Unaweza kuchangia vipimo kwa Kufanya kipimo cha OONI Probe katika nchi yako. Njia rahisi zaidi kufanya vipimo ni kwa kutumia programu ya simu ya OONI Probe katika Android na iOS.