Seti ya huduma ya OONI
Ushiriki wa jamii ni moyo wa kazi za OONI, kama OONI data kwenye udhibiti wa mtandao inategemea na upimaji wa watu OONI Probe ulimwenguni.
Umevutiwa kushirikisha jamii yako na kipimo cha udhibiti cha OONI?
Seti ya huduma ya OONI inajumuisha nyenzo ambazo unavutiwa kuzitumia kama sehemu ya juhudi za ushiriki za jumuiya ya OONI.
Vipeperushi vya OONI
Tumetoa Vipeperushi vya OONI viwili 2 ambavyo vina taarifa kuhusu
utumiaji wa vifaa vya OONI na data kwa ajili ya kuchunguza udhibiti wa
mtandao ulimwenguni.
Kanzi data ya OONI Probe
OONI Probe ni programu ya bure kwa ajili ya kupima udhibiti wa mtandao.
Kushirikisha watu kwa kutumia OONI Probe, tumetoa Kanzi data ya OONI
Probe ambayo inaweza kusaidia kutoa taarifa ya jumla kuhusu OONI Probe,
na kuhimiza kupima kuelekea au wakati wa uchaguzi (wakati matukio ya udhibiti yanayojitokeza).
Kanzi data ya OONI Explorer
OONI Explorer ni kanzi data huru kubwa
zaidi duniani katika udhibiti wa mtandao. Kuhumiza utumiaji wa OONI
Explorer, tumetoa kipeperushi cha OONI Explorer.
Kipeperushi cha Udhibiti wa mtandao
Kupitia kipeperushi hiki, tumetoa baadhi ya taarifa muhimu kuhusu
udhibiti wa mtandao na kwa namna gani udhibiti wa tovuti hufanyika.
Maudhui ya semina za OONI
Una nia ya kuwezesha semina na OONI?
Tumetoa maudhui ya semina ambapo unakaribishwa kupakua na kutumia
kutokana na mahitaji ya hadhira yako. Maudhui haya ni muongozo,
tafadhali usiyachuckulie kama ni maudhui ya uwasilishaji ya mwisho.
Tunahimiza kila mmoja ayatumie kwa muktadha wa mazingira ya nchi
anayoratibu tukio, na mahitaji ya hadhira yako.
Shukrani kwa juhudi za kutafsiri za Advocacy Assembly tumeweza kutoa
maudhui pamoja na maelezo ya wasemaji katika uwasilishaji.Tunatumia
maudhui haya yatarahishisha katika maandalizi ya semina yako, na
itafanya maudhui haya yaweze kupatikana zaidi kwa hadhira yako.
Pia unaweza kujisajili bure katika kozi ya mafunzo ya OONI ya mtandaoni
katika tovuti ya Advocacy Assembly ambayo inapatikana kwa Kiswahili.
Rasilimali za OONI
Itakua bora kwa kurejea katika maswali yanayoulizwa mara kwa mara (MYM) na vipengele vya faharasa kwenye tovuti yetu.
Tuna tumai umepata rasilimali muhimu za huduma za OONI! Kama una maswali yoyote au mapendekezo ya namna ya kuboresha seti ya huduma, tafadhali tutafute.
Tunakushukuru kwa juhudi za ushiriki wa jumuiya ya OONI, na tunawashukuru Ura Design
kwa muonekano mzuri wa seti ya huduma ya OONI na Zaina Foundation kwa kutafsiri seti ya huduma ya OONI kwa Kiswahili.