Seti ya huduma ya OONI

OONI Outreach Kit

Ushiriki wa jamii ni moyo wa kazi za OONI, kama OONI data kwenye udhibiti wa mtandao inategemea na upimaji wa watu OONI Probe ulimwenguni.

Umevutiwa kushirikisha jamii yako na kipimo cha udhibiti cha OONI?

Seti ya huduma ya OONI inajumuisha nyenzo ambazo unavutiwa kuzitumia kama sehemu ya juhudi za ushiriki za jumuiya ya OONI.

Vipeperushi vya OONI

Tumetoa Vipeperushi vya OONI viwili 2 ambavyo vina taarifa kuhusu utumiaji wa vifaa vya OONI na data kwa ajili ya kuchunguza udhibiti wa mtandao ulimwenguni.

Kanzi data ya OONI Probe

OONI Probe ni programu ya bure kwa ajili ya kupima udhibiti wa mtandao. Kushirikisha watu kwa kutumia OONI Probe, tumetoa Kanzi data ya OONI Probe ambayo inaweza kusaidia kutoa taarifa ya jumla kuhusu OONI Probe, na kuhimiza kupima kuelekea au wakati wa uchaguzi (wakati matukio ya udhibiti yanayojitokeza).

Kanzi data ya OONI Explorer

OONI Explorer ni kanzi data huru kubwa zaidi duniani katika udhibiti wa mtandao. Kuhumiza utumiaji wa OONI Explorer, tumetoa kipeperushi cha OONI Explorer.

Kipeperushi cha Udhibiti wa mtandao

Kupitia kipeperushi hiki, tumetoa baadhi ya taarifa muhimu kuhusu udhibiti wa mtandao na kwa namna gani udhibiti wa tovuti hufanyika.

Maudhui ya semina za OONI

Una nia ya kuwezesha semina na OONI?

Tumetoa maudhui ya semina ambapo unakaribishwa kupakua na kutumia kutokana na mahitaji ya hadhira yako. Maudhui haya ni muongozo, tafadhali usiyachuckulie kama ni maudhui ya uwasilishaji ya mwisho. Tunahimiza kila mmoja ayatumie kwa muktadha wa mazingira ya nchi anayoratibu tukio, na mahitaji ya hadhira yako.

Shukrani kwa juhudi za kutafsiri za Advocacy Assembly tumeweza kutoa maudhui pamoja na maelezo ya wasemaji katika uwasilishaji.Tunatumia maudhui haya yatarahishisha katika maandalizi ya semina yako, na itafanya maudhui haya yaweze kupatikana zaidi kwa hadhira yako.

Pia unaweza kujisajili bure katika kozi ya mafunzo ya OONI ya mtandaoni katika tovuti ya Advocacy Assembly ambayo inapatikana kwa Kiswahili.

Rasilimali za OONI

Itakua bora kwa kurejea katika maswali yanayoulizwa mara kwa mara (MYM) na vipengele vya faharasa kwenye tovuti yetu.

Tuna tumai umepata rasilimali muhimu za huduma za OONI! Kama una maswali yoyote au mapendekezo ya namna ya kuboresha seti ya huduma, tafadhali tutafute.

Tunakushukuru kwa juhudi za ushiriki wa jumuiya ya OONI, na tunawashukuru Ura Design kwa muonekano mzuri wa seti ya huduma ya OONI na Zaina Foundation kwa kutafsiri seti ya huduma ya OONI kwa Kiswahili.